Akasema: Hebu nambie khabari ya huyu uliye mtukuza juu yangu. Ukiniakhirisha mpaka Siku ya Kiyama, hapana shaka nitawaangamiza dhuriya zake wasipo kuwa wachache tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Iblisi akasema akionesha ujasiri wake na ukafiri kwa Mwenyezi Mungu, «Unamuona kiumbe huyu uliyemfadhilisha juu yangu? Ukinibakisha hai mpaka Siku ya Kiyama nitawatawala wale wanaozalikana na yeye kwa kuwapoteza na kuwaharibu isipokuwa wale waliotakaswa katika Imani, nao ni wachache.»